Pageviews last month

Tuesday, March 22, 2011

HOJA JUU YA TIBA YA MCHG. MSTAAFU HUKO LOLIONDO TZ

ASANTE SANA MTUMWA MWAMINIFU ISAAC KWA KUTUPA HIZI DODOSA...
Nashukuru kwa muda wako, nimesoma kwa uaminifu jinsi umejaribu kutupatia mahala pa kuendelezea udadisi juu ya tiba hii tata ya loliondo.
Nikiunganisha na maswali ya msingi yaliyotangulia nafikiri tunahitaji sasa HEKIMA za waalimu na uongozi thabiti wa Mungu juu ya hili.

Kwanini wengi hatupendi kulizungumzia hili
Kwanza ni: sababu ya kutokuwa na uhakika na majibu au hisia tulizo nalo juu ya hili..

Pili ni: kutotaka kumpotoa msomaji kwa shauri au majibu yetu.. Je! kukaa kimya ni sahihi? sina uhakika.. Ila tunajifunza mara nyingine kukaa kimya huesabiwa kuwa hekima kwetu japo pia twajifunza kuwa kunena hujenga hekima za midomo yetu..

Tatu ni: kutaka kuwa makini saana, na kuogopa kusema kwamba sasa tutaonekana aje!! kama kituko hivi yaani mimi mtumishi mzima natetea madawa ya kimapepo, hata sishuhudiwi kabisa na 'loho' wa bwana... na labda kuhofia kupoteza infuelnce.... lol this is fun but i think it can be very true!..

Kaka ISAAC M MPATWA nishukuru kwa hii scheem uliyoituma hapa, nikutake radhi kwa usumbufu wa andishi zetu za kiholela.."free writing" mtuwie radhi na wengine wote.. sasa kwa msaada wako ninatumia hii kujibu kidogo na kuuliza na kujieleza...samahani kama ntakuwa sitoi jibu kama ulivyotangulia kuhoji...
Pia nakutoa wasiwasi kwamba usijali kusema kwamba mpaka sasa hakuna aliyetoa jibu la moja kwa moja naamini hakuna atakayekuwa offended maana hata jinsi ambavyo hujaamua kutoa jibu hapa kila mtu atajisikia okay tuu... lol

Nianzie hapa
SERIKALI:
Swali: Serikali ingeomba ushauri kwa kanisa ambalo ni mimi na wewe. Nisingejibu Amani ya Kristo Iamue mioyoni mwao!! lol.. Hili lilikuwa ni jibu kwa sisi waamini tulipokuwa tukihojiana sisi kwa sisi... maana nilikuwa nashangaa kwanini tutake kuulizia kwa wengine,, kama ni hivyo basi twende kumuuliza babu mwenyewe..
Ila kwa serikali jibu nafikiri ni hili hitimisho:
NAKUBALIANA NA HITIMISHA LAKO KWA NYINGI KAMA SI ZOTE... Hichi ndicho pia tukiulizwa na Serikali tunaweza kushauri... Kwa hili limekaa sawa kiroho, kiakili na kivingine:
Tiba ya Babu inahitaji kufanyiwa utafiti zaidi badala ya watu kutumbukia tu kwenye kuamini kwamba huko Loliondo kuna miujiza inaendelea. Kazi ya wanazuoni ni kufanyia utafiti kila jambo ili lieleweke. Wenye imani waendelee na imani zao, lakini taaluma ichukue nafasi yake ili tufahamu wapi mambo yanaishia. Hata wagonjwa walioponywa na Yesu waliweza kuthibitika kwamba wamepona, mathalani
vipofu. Si lazima kuijua miujiza ya dawa, bali ni lazima kujua iwapo ni kweli wagonjwa wamepona.
Mimi naona hili ni jibu kwa upande wa serikali hivyo itoe support ntakayohitaji ili nikamilishe tafiti zangu...ambazo kwa upande wa kiroho sitakuwa na kazi kubwa sana..

Narudia kusema kwamba kipindi fulani nilitaka kushawishika kwa mguso wa "Ki-Relativism" kwa huyu Babu anaweza akawa yuko sawa...
Pale ambapo niliona Serikali inataka kukataza... Nihusisha na mambo kadhaa ambayo niliwahisikia kuwa serikali huwa inakubali mamboyanayokuwa hasara tu kwa nchi na wananchi wake mfano vyakula vibovu huwa vinaingizwa nchini bila shida, majawa yaliyokwisha muda wake hakuna shida, madawa ya majaribio bila uanngalizi mzuri, maziwa mabovu ya watoto hakuna shida, mikataba mibovu mingi na ya gharama kubwa hakuna shida, mingine inasainiwa nje na wananchi hawaruhusiwa hata kujua japo ni nchi yao nk... hivyo nikaona hakuna historia ya kupitisha yaliyo mema hivyo hichi wakatazacho labda kina kheri ndani yake!! Hata hivyo bado sijafahamu maana walikuali iendelee kwa shinikizo kama inavyotokea kwenye vitu vingi




Matokeo/ Result: mwisho wa neno waweza kuwa kipimo chema cha swali hili ndo maana kautafiti kanahitajika... mtu akizungumzia kwamba angependa kufika hapo mahala pa interest ni shabaha mojawapo ya kuanza kudadisi na kutafiti anachokisikia yamkini hata kukiamini...

KANISA:
Kwa Upande wa Kanisa au waamini, sidhani kama tupo kwenye nafasi nzuri sana ya kulijibu hili kwa sababu ya misingi tuliyonayo.... ni ngumu kidogo kuanza mazoezi wakati wa vita.... ndo maana ninashangaa kwanini tunashikia bango swala hili tuu... inamaana lipo hili tuu lenye utata Tanzania yote au...Kaka Boaz Aron hauna taarfia yoyote toka huko Mkoani!! Kuna utata mwingi kila kona!!! Nafikiri hii haitoi uhalali wa kukaa kimya ila...
Kanisa linawezekana kuonekana kuwa biased kama litaishia kukosoa kazi ya babu tuu na kwa njia hiyo hata zile Imani nyingine zilizopo zinazosadikiwa kuwa ni za giza zitatumia mwanya huu kuona zimesafishiwa njia kwamba ziko sawa!!
Kwa Kanisa kulifanyia uspeciality swala la lolionda na kuonesha kwamba ndiyo lina Ukibwetere mkuu, na ndiyo swala la kuumiza vichwa sana, kwangu ndiyo moja kati ya vitutu vinavyonitatiza sana... Nafikiri pako technical kidogo tu, lakini pana umuhimu wake mkubwa!!

Binafsi Kama Kanisa Nafikiri ni sawa kuiambia serikali inatakiwa ifunge na kuomba kama huo ndiyo ujumbe aidha wa kinabii au ni neno la maarifa sioni kama kuna shida kuwaambia wafunge na kuomba hata kama wao ni wagirsashi na wayebusi...kwani hamkumbuki kuwa Ninawi walitobesha mpaka mifugo yao siuze hawa wazaliwa wa nyama...sasa Kama watakataa hilo ni swala jingine...
Kama uponyaji au jibu liko kwenye kufunga na watafunga... Mbona huwa wakienda kwa waganga wanaambiwa wale majivi na wanafanya hivyo siuze kufunga!!

Kukaa nyutroo ni sawa kama huna jibu omba!!

Pia mimi nahisi kama sijasikia jibu la moja kwa moja juu ya hoja hii, lakini inawezekana imeshasemwa ila mikao yetu na stahili zetu hatujang'amua...
Maana kama litakuwa ni la Bwana si Mungu anasema hatafanya kitu chake mpaka amewaambia mitume wake maanabii

Swala la kwenda Loliondo physical..ni mojawapo ya jambo la kitafiti...kama unavyoshaauri pamoja na ukiroho wake ni aje kama rohoni juu ya swala hili unajisikia kufika huko

Kama Rais angekuomba ushauri...Ningejibu kama nilivyojibu hapo kwamba ningependa kwenda... na taratibu za kuliangalia kitafiti kama ulivyopendekeza lingekuwa kitu cha pili ili kuweza kushawishi kada zote... Kwamba ni swala la Kiroho lakini Napenda kuuthibitishia Umma kwamba mwenyewe nimelishuhudia...
Sizani kama Rais au Dola ambayo inahitaji jibu yakinifu haitakuwa tayari kusikiliza resoultion yako na approach katika swala lililokuwa na utete mkubwa kwao na wananchi wake.

RESEARCH PROPOSAL

MUHIMU:
1. Kila nadharia iangaliwe yenyewe bila kuihusisha na nyingine.
2. Malengo ya Babu si mjadala katika nadharia tete hizi.
3. Imani za watu, washabiki ama wagonjwa wa Babu si sehemu ya nadharia hizi.
Vidokezo vinavyouunga mkono kwamba hii ni tiba ya kiroho:

1. Kwamba Babu amesema hivyo na tunatakiwa kumwamini bila maswali.
HILI SIJALIELEWA LINA MAANA GANI HASWA...Kama nimeelewa nazani si kutouliza au kuuliza swali inatoa uthibiti kuwa i swala la kiroho au kimwili
2. Alikuwa mchungaji wa kanisa linalomwabudu Mungu la Kilutheri.
SIZANI SANA KAMA NI CREDIT... KWANI YUDA NAYE ALIKUWA NI MMOJA YA WANAFUNZI WA YESU LAKINI ALIMSALITI
3. Anafanyia dawa yake maombi kwa kumtaja Mungu.
SWALA LA KUHAKIKI NA MUNGU YUPI ANAYEMUOMBA NDIYO NILISEMEA NI UHUSIANO WA MTU BINFSI NA MUNGU WAKE...kama ni Mkristo ndo hapo mahala pema pakupambanua... B

Binafsi sidhani kama Mkristo aliyendani ya YESU hata bila kung'amua kama huyo mchungaji anatumia nguvu za giza ati ukiomba naye na wewe Imani yako Iko kwa Mnazarethi utaingiwa na wadudu...Hili Siliamini hata Kidogo...Nimekataa....Ntaandamana... Nisaidieni wapendwa hapa na wadada....
Najua tuko Sealed na HolyGhost mwenyewe...
Siko na Madharau najua nafsi za waamini mara nyingine hushikwa na fahamu zao...katika mitengo ya namna namna ... Lakini hapa nahitaji msaada... waamini...
Mmeshawahi kumsoma Jamaa mmoja alikuwa anaitwa "William Marrion Branham" mtafuteni huyu mmsome kidogo na bio yake wenye kiu ya kuchimba chimba juu ya yanayojiri loliondo na yafananayo na haya...Lazima tuweze kusimama wenyewe... kama tunataka kuendelea

Vidokezo vinavyopinga uwepo wa tiba ya kiroho:

NAFIKIRI HAPO UNGEFAFANUA VINAVYOPINGA UWEPO WA TIBA YA Kiroho kipi.. NAFIKIRI BINAFSI NIMEKUPATA LAKINI TUFAHAMU Kishetwani ni kiroho vilele..SIYO KIMWILI au siyo?

3.Kufanya maombi bila kumtaja Yesu kunazua maswali mengi.
HILI NDO MOJA YA MAMBO AMBAYO NINGEPENDA KUTHIBITISHA... Niliseme mahali pengine kuwa kutaja Jina la Yesu ni Vizuri...
Lakini sidhani kama hilo tuu latosha.... Maana Yesu mwenyewe alisema kuwa wata kuja makristo wengi.. sasa anaweza akatumia pia jina...
Naelewa umeweka hizi points za kutrace tuu!! ni sawa

> 4. Bei ya dawa kuwa ndogo inaweza kuwa ni mkakati wa kibiashara ili kuvutia watu wengi na kuwafanya wawe na imani.
NAFIKIRI BEI NDOGO PIA INAWEZA KUFANYA WATU WAKAWA NA SHAKA NAYO PIA...

JE HUJAFIKIRI HII INAWEZA KUWA KAMA MATOLEO/SADAKA
Tunavyokuwa tunaambiana au kuambiwa tupande mbegu juu ya swala fulani,Tunafanya hivyo na vitu vinatokea kuna shida gani...
PENGINE NILISEMA KWAMBA Kama tunahoji kuwa kapewa bure na atoe bure....Ila kuna wahudumu wa hiyo madhabahu yake wanahitaji kula madhabahuni naye halikadhalika ili asiende kuiba.... kuna vifaa vihitajivya gharama pia sasa inakuwaje hapo juu ya gharama!!! Hivi wale NUWA au 'DAWASA' ya loliondo ikikata maji pale itakuwaje... babu analipa bill yule au?

5. Biblia inaonya kwamba katika siku za mwisho wataibuka watu wa miujiza kama Babu na watapotosha hata wateule.
HII NI NZURI SANA NA HAPA NINA SWALI... BINAFSI SIJAONA MAHALA AMBAPO HUYU babu anawa-"bind" au anawafunga watu kwa maagano fulani fulani na kama kuna masharti yoyote yanayoonesha kama kuna connection na kumrubuni mtu na Imani yake niambiwe...
Maana kila mtu anakwenda na kupata dozi kisha anaondoka...

NAOMBA SANA NISAIDIWE NA HILI... Maana huko kwenye nyumba za Ibada nyingine ndo huwa hata tunaambizana hapa ndo mahali pakustailipo...Kaa Hapa hapa ili utunze uponyaji,,,kaa hapa tukufunde.. sisemi kama napingana na hayo... lakini kama kuna tashwishi tungeanzia huku kwetu tunakoambianaga kwamba usiende kule huwa hawaokoki!!! khe Karne hii jamani!!
Kipindi fulani tuliendaga mahala fulani na marafikir zangu tukafanya uinjilisti wee watu wakaokoka wengine wakaponya na kufunguliwa na mambo mbalimbali...tukawakabidhi hawa wachanga kwenye kanisa fulani wakafurahi kweli...baadaye kutaka kufahamu tunaabudu kwenye viota gani!! wee... wakasema inabidi woote tutoke huko... samahani hapa kama ntakukwaza yeyote maana nasikia bado mahubiri haya ni deal hata sasa... hii ni kazi kweli kweli

Nadharia Tete II: Tiba ya Dawa ya Kienyeji
MiMi NAAMINI HATA DAWA NYINGINE KAMA KLOROQUINE, ASPRIN, BUTAZOLD NK. Zote hizi wanadamu hupewa ufunuo wa kiuchunguzi na Mungu katika kiwango fulani cha Maarifa...
Sasa ya Babu labda kwa sababu haijapita kwenye njia za kisayansi na kuthibitishwa kimaabara... Inaleta utata kwasababu ya u-kiroho wake au 'udivain' wake!! Utata ruksa hapo!

Rejea za kwenye magazeti ulizonukuhu wapo waliopona na waliokufa..
Binafsi ningeshauri kutazamwa waliopona..Hao ndo sample za kungalia kwa mfano kuna ugonjwa ambao ilionekana kama Dawani wamefikia Kikomo...Lakini Mara baada ya kutumia tiba za Babu wakapona ndo inabidi tuwaangalie...

Kwanini nasema hivi... Nina SABABU KUU TATU:

MOSI: Ni kwamba mwisho wa maisha ya kila binadamu ni kifo... Hivyo haithibitishi kufa kwa yule mpendwa ni sababu dawa haifanyi kazi... Sababu watu hufikiri kinachomuua mtu ni ugonjwa!! haha.. Kifo ndo humuondoa mtu uhai..

PILI: Huyu mgonjwa anaweza kuwa amepona kabisa huo ugonjwa unaitwa ni Ukimwi labda lakini anakufa sababu kifo kimekuja na ujue anakufa na nini... labda malaria,, au hata kama alikuwa ana kisukari anakufa siku hiyo na mafua...

Sasa hapo nisichanganye na kwanini dawa hii hutibu baadhi ya magonjwa tuu... Ndo alivyopewa kama karama mbalimbali

Kwani wewe hata kama unaomba upone ndui... halafu una kichocho usipopona uta-complain?

MWISHO:Ni Mwanamume Yesu Kristo peke yake ndo alikuwa haudhurii maziko, wala misiba, Yeye alikuwa mshinda mauti by nature..kwake mapepo (mizuka, mizimu-zimwi na majini) hayakusimama...
Sasa kumlinganisha Babu na mwanamme Yesu sijui inakuwa aje hapo...nafikiri na sisi tujaribu pia kujifananisha naye .maana si ndo tunataka tuwe hivyo na kuumbwa kwetu kwa mfano wa Mungu...
Ikumbukwe Ktk hili narudia hata mahosipitalini na madawa yaliyotafitiwa na kuthibitishwa watu hufa...kwa hiyo kufa isiwe kipimo kwani Babu si Yesu..
Pia nafikiri babu hajasema ukinywa tuu lazima upone...nafikiri alisema inatibu... mtu mpaka kufikia uponyaji kamili ni process iwe kiroho au kimwili....

Kwamba anaegemea Dawa ya Kienyeji sijaelewa kidogo, inamaanisha nini!!
Yaani kuna dawa ya kienyeji na ya kigeni... na kati ya hizo kuna iliyo superior zaidi ya nyingine au?

4. Babu ana orodha ya magonjwa yanayotibiwa na dawa hii: UKIMWI, Pumu, Kisukari,
Shinikizo la Damu, na Saratani. Huu ni utaratibu wa dawa za kienyeji kwamba...
KWANINI MUNGU ACHAGUE MAGONJWA MACHAHCE... Hapo sijui kwanini hivyo..
HIVI NI KWANINI PAULO ALIMWAMBIA TIMOTHEO ANYWE MVINYO kwaajili ya tumbo lake KWANINI HAKUMWAMBIA ANYWE kwaajili ya kifaduro, tetekuwanga, kichomi, mkanda wa jeshi, kipanda uso, kaswende, Degedege, Surua na mengine yote?

5. Babu anasema kwamba mgonjwa anahitaji kusubiri kwa wiki tatu kabla ya kuangalia afya yake. Yesu alipoponya watu kwa uwezo wa Mungu, walipona hapo hapo. Kusubiri siku kadhaa ni utaratibu wa dawa za kienyeji (na za kisayansi)
HAPO SIJUI KWANINI WATU WANAPEWA PROBATION... INAWEZEKANA NI YEYE MWENYEWE BABU anavyojisikia...Kitu ambacho hutokea hata kwa watu wa Mungu wa kweli kabisa Mungu anamtumia mtu katika jambo fulani halafu analowea anaanza kufanya kwa mazoea na kujitwalia utukufu na vitu kama vile

Vidokezo vinavyopinga kwamba hii ni dawa ya kienyeji:
1. Madai ya Babu kwamba kuna neno la Mungu ndani ya mti. (Dawa za kienyeji hazibebi maneno ya Mungu).

2. Babu anasisitiza kwamba ni lazima aiombee dawa hiyo, hivyo anaitoa katika orodha ya dawa za kienyeji.
HAPO INABIDI ITAFSIRIWE UNAVYOSEMA DAWA YA KIENYEJI UNAMAANISHA NINI? Kienyeji kinyume chake ni kigeni au kienyeji kinyume chake ni kitaalamu/Kisayansi/Kisasa... Au Kienyeji ni Kiasili....Au Kienyeji ndo ile wanasema ni ya Kichawi/ Kishirikina??

3. Masharti ya Babu kama kukupa yeye tu, na mengineyo yasiyokuwa sawa na ya kienyeji, yanashawishi nguvu zingine.
SASA HAPA TATIZO LAKE NI NINI? Nauliza tuu.. msinipige jamani
Sishawishiki eti sababu kuna masharti ndo inahusika na nguvu za giza... labda yatajwe mashati hayo ni yepi
Mifano ya Masharti niliyowahi kusikia kwenye vitabu vya Mungu:
Musa piga maji mara kadhaa uone nini kitatokea..
Enenda na usitende dhambi tena hilo ni sharti ukitenda litakalotokea shauri yako..
Au enenda na usigeuke nyuma hilo ni sharti uikigueka usije laumu mtu buree..
Nenda ukawaambie tuu yale uliyoyaona hili ni agizo..
Pakeni damu katika miimo ya nyumba zenu hilo ni sharti ili kupona..
Zungukeni Ukuta wa Yeriko Mara Kadhaa kuangusha hilo kuta...
Jemedari Naamani Nenda kanawe mara kadhaa kuponya Ukoma wako.

Sasa na haya si ni masharti, kwa hiyo twaweza kusema kama huu ni uchawi/ ulozi au tuseme hii ni nini? Najaribu kuiingiza akilini ikae, ila inanitatiza kiasi.

Maana mara nyingine na sisi huwa tunachagua mahala pa kuabudu, counseling, Maombezi na labda Mtu fulani kwamba anatumia na Mungu sana katika eneo fulani...
Sasa hapo Kama Kanisa Mnamuuliza Mungu... Mimi sina shida ukiniuliza ntakujibu hivyo...
Na Serikali Ikiniuliza Ntaijibu ni Swala la Kiroho..Serikali inajua maswala ya Kiroho yapo na ndiyo maana huwa inaomba maombi iombewe na watu wa kiroho... Hata kama ikiwa ni fisadi au chafu ya kutapikwa!!

4. Bei ya dawa ni ndogo kuliko dawa za kienyeji zingine.
SIJAFANYA TAFITI YA DAWA ZA KIENYEJI...ILA KWA neno LAKO NAAFIKIANA NAWE TU ..mambo ya price regulation na ushindani wa kibiashara

5. Magonjwa anayotaja Babu ni mengi mno kuweza kutibiwa na dawa moja kwa kuwa yana vyanzo tofauti, yaani etiolojia.
HILI LINAWEZA KUWA NA KUJICHANGANYA NDANI YAKE,, NAFIKIRI LIKO VERY FLEX... Kama litakuwa limenipelea lakini

Nadharia Tete III: Tiba ya Nguvu za giza Kwamba Babu anatumia nguvu za giza, kwa maana ya uchawi/ mashetani/ maruhani/majini ama pasipo kujua au hata huku akijua na kisha kumhusisha Mungu ili kupumbaza watu, hivyo watu hawaponi bali kuna uwezo wa kishetani unaotoa nafuu ya muda na pengine kuwapoteza akili wanaowapima wagonjwa hawa (kama wapo) mara baada ya kutumia dawa.

INAWEZEKANA NI KWELI HOJA HII.. NIULIZE SWALI...
Nini apatacho Shetani juu ya hili?
Je! anakuwa ameabudiwa, amesujudiwa au nini? Kama hilo ni Jibu hiyo yaweza kuwa athari kweli!! Nakubali....
Lakini swali la nyongeza kwani kuna tofauti gani kama hawa watumiaji ni kawaida yao kwenda kwa waganga wanaotumiwa na Ibilisi na Majini?
Nafikiri hii si itakuwa ni moja tu kati ya hayo mapito yao!! Maana ni kawida yao kwenda kwa wachawi sasa leo nini jipya kuna geni gani?

NA HII HAPO JUU NI MOJA KATI YA HOJA ZANGU KWANINI KWA BABU WA LOLIONDO TU... NDIYO KANISA Litakiwe kusema wakati kuna mengi tuu!!
Je! Hatutakuwa wanafiki sisi... Au ndiyo tunaanzia kwa babu tutaendelea mpaka mwisho wa Nchi!!

Naomba niambiwe pia Mtu anaathirika aje akitumia hii Dawa... Kiroho, Kimwili na Kiafya...
Binafsi ningeiambia Serikali mpaka sasa sijaona athari zake za Kiroho ila nipeni muda nifanye tafiti kuhusu Kiafya kunakohusisha miili na akili kama sijakosea

Angalizo: Hili si jambo geni Tanzania na hata nje ya nchi na mafundi wa kazi hii ni wachawi, wachungaji na mashehe na wapo siku zote).

Vidokezo vinavyouunga mkono uwezekano wa kuwepo ushetani:
1. Hadithi za ndoto za Babu ambazo zinafanana na wanazoota wachawi kwa madai kuwa ni Mungu ndiye amewaotosha.
2. Kumtaja Mungu haina maana ni MUNGU huyu tunayemjua sisi; huenda anamaanisha "mungu" anayemjua yeye.
3. Msururu wa masharti kama wafanyavyo wachawi, n.k.
4. Mkusanyiko wa magonjwa mengi kwa pamoja na yote kutibiwa kwa dozi hiyo hiyo ya kikombe kimoja.
5. Historia ya kuwepo waganga wanaofanya uganga na uchawi kwa pamoja, yaani dawa za kienyeji na vioja vya kishirikina.

HAPA NAKUMBUKA ULIANGALIZA KUTOFANANISHA NADHARIA MOJA NA NYINGINE...LABDA NAJICHANGANYA MWENYEWE NISAMEHEWE KAKA!!
Ila nifahamuvyo mie siyo sye "TUKOPIO" Vitu Toka kwenye ufalme wa giza ila ufalme wa giza ndiyo hukopi vitu toka kwetu kwa "ASILI"...nasema kwa "ASILI" Ibilisi ndiye hujigeuza kama malaika wa nuru... Sasa kama Swala la kuota ndoto sizani kama lilianzia kwa wachawi... Wote tunafahamu habari za kina Yusuphu Muota ndoto na wengine waliokuwa wanafunuliwa ndoto kama Mtu wangu Danieli... Kama kutakuwa na chronological challenge...Niseme kimaandiko inasomeka hivi na vijana wenu wataona maona na wazee wenu wataota ndoto!! au inakaaje hii?

Kwamba kama Dawa ya Babu inatibu zaidi ya Ugonjwa Mmoja,, Hivi kwetu ni nani aliyewahi kuishi Tanzania na wimbi kubwa la mbu wale kama hajawahi kunywa muarobaini...sasa huu mche wa kondeni huu inasemekana unatibu kama magonjwa arobaini!! TATIZO ni nini juu ya mti huu...40 inaweza kuufanya ukawa na uwalakini?

Uko mti mwengine unaitwa Mratuni.." Ni Antibayotik" ya kiasilia/ kienyeji...ile inatibu vidonga, tumbo "vyro", Kideri kwa kuku, macho nk... Mimi nilishaitumia... ilikuwa ni-garantii nikiumia kwenye michezo ya mpira huko nimechunika..ni garantii siku tatu niko fit...sasa hata wewe ukija nakwambia Guarantee siku tatu utakuwa fit....Utanipeleka mahakamani?
Nauliza tuu kwa mfano?

Vidokezo vinavyopinga uwepo wa nguvu za giza:
1. Dawa za kienyeji zipo na zinatibu kweli hata zikiwa peke yake bila uchawi wala maombi.
HAPO SASA NI DAWA YA KIASILI NAFIKIRI TUNAWEZA ITA HIVYO...maana hii kienyeji mara nyingine nimeona hata unapoandika ukisema kienyeji tuu tayari unawakilisha ya kichawi!!! NILIOMBA TUTAFSIRI neno "KIENYEJI"
inatumika aje? ina maanisha nini hasa kwa mtungo wetu wa kisasa

2.Si rahisi mchungaji kujishughulisha na uchawi, kwa kuwa wachungaji ni watumishi wa Mungu.
YES / NO... Ibilisi alikuwa Malaika Mkuu wa Sifa

3.Kwa kuwa Babu anamhusisha Mungu na kuna imani za watu kwa Mungu, basi si rahisi mashetani yaka hapo kijijini.
Shetani alipoulizwa anatoka wapi akasema natoka HUKU, HUKO NA HUMO!! I give a benefit of doubt on this!!

4.Uponyaji wa Mungu (enzi za Yesu) unaweza kufananishwa na uchawi kwa sababu binadamu hana akili za kuuelewa.

NI KWELI KWA SEHEMU LAKINI SASA KAMA KATIKA HILI TUNALO NENO Kwa maana ya ANDIKO na ndicho tukifanyacho hapa mpaka mwisho wa siku kitakuwa kishaeleweka

5. Kuna watu wachache wanaodai walitibiwa zamani na wameshapona, mmoja ameripotiwa na gazeti la Mwananchi katika siku za nyuma kwamba anafanya kazi kwa Babu na amepona Kisukari.

HUYU TUNAHITAJI REKODI ZAKE ZA AWALI NA USHAHIDI WA WATU WANAOMFAHAMU
Hii ni Kitabibu kawaida kabisa kama hakuna rekodi siyo Sample nzuri

HITIMISHO:
Tiba ya Babu inahitaji kufanyiwa utafiti zaidi badala ya watu kutumbukia tu kwenye kuamini kwamba huko Loliondo kuna miujiza inaendelea. Kazi ya wanazuoni ni kufanyia utafiti kila jambo ili lieleweke. Wenye imani waendelee na imani zao, lakini taaluma ichukue nafasi yake ili tufahamu wapi mambo yanaishia. Hata wagonjwa walioponywa na Yesu waliweza kuthibitika kwamba wamepona, mathalani
vipofu. Si lazima kuijua miujiza ya dawa, bali ni lazima kujua iwapo ni kweli wagonjwa wamepona.

Kwamba taifa linapotea ujingani, umaskinini, na maradhini hilo linafahamika.. Sidhani kama babu ndiyo "FUNGUO" wa huu upotevu wa Taifa lenye zaidi ya miaka 50... na Idadi ya watu wakisiwao kufikia milioni 40
Mimi nisingependa kabisa Tanzania iendelee kupotea.. Nasukumwa kwamba hatuko kwenye njia sahihi kwa mengi saana... Ila Hili la Loliondo kuchukulia kuwa ndiyo linaifanya Tanzania ipotee!! Sasa dukuduku langu ni kwamba inapotea upotevuni au inapotelea wapi?
Maana to be real we are far from the TRUTH..Ambaye ni YESU... nikisema kwamba tunatakiwa tuijue kweli nayo kweli itatuweka huru watu watauliza sasa hilo ndilo nitakaloishauri Serikali? Yes, especial kwenye suala kama hili.. It's our Opportunity to speak out about TRUTH na habari ya tumaini letu... tena tumeulizwa bwana why not!!
Huwezi kuwaambia amani ya Kristo iamue mioyoni mwao, ni kweli maana hujui hata utakayeongea naye.. maana ziko amani nyingi,, hata tukitaka kuwaambia kuhusu hekima ziko hekima nyingi... know them..Tutaanzia pale walipo... Ni vyema pia Kujua mtazamo ikitokea ukaulizwa na Serikali...
Ni vyema ukajua huyo aliyekuja kwako ana ulewa kwa kina gani juu ya Hilo atakapojieleza nawe ndiyo uanze kujipambanua...
Ndo maana nimesema kule mwanzo yatupasa tuombe Hekima...na nimeomba waalimu pia waseme neno...Samahani kama nilieleweka Kijuujuu hivyo na kirasharasha hivyooo...
Mimi niko tayari kuhojiwa na serikali.... kupitia scheem hii...nimejiridhisha...
Sasa siwezi kukujibu wewe sababu wewe si Serikali....
Nimejaribu kulijibu kanisa...
NIMELIKUBALI HITIMISHO

NIKUSHUKURU MTUMISHI KAKA ISAAC M. MAKALA KWA KUTUSAIDIA KUWEKA SCHEEM YA KIUSADIFU WENGINE TUNAJUA KU-FIX A/C, CARBURATOR NA TURBINE lol

Wednesday, March 16, 2011

MIJADALA YA TIBA YA UKIMWI NA MAGONJWA SUGU ARUSHA LOLIONDO

WANAVYOKABILIANA NA UJIO WA TIBA HII ITOLEWAYO NA MCHG. WA HUKO LOLIONDO...
BINAFSI NAHISI KUNA AMBAO WANAONGEA WAKIWA NA BITTERNESS NA INATOKEA WAPI SIJUI, ILA NINA DUKUDUKU KIDOGO...
LEO NIONGELEE MAMBO MATANO:
/MMEPEWA BURE TOENI BURE, BABU HAJAPEWA VITENDEA & WATENDA KAZI BURE!
/KUHUSU UTUMIAJI WA JINA LA YESU KRISTO.
/NENO LINATUFUNDA NINI JUU YA KULAANI? BARIKINI WALA MSILAANI
/KUHUSU KUZIPIMA "roho", HATA BINFSI TUJICHUNGUZE
/MUNGU ALITUPA MUONGOZO JUU YA VYAKULA, VYAKUNYWA NK.(Uponyaji kwa vitu vya asili)

MMEPEWA BURE TOENI BURE... NI KWELI ILA HUYU BABU KAPEWA TIBA BURE ILA HAJAPEWA WATENDA KAZI NA VITENDEA KAZI BURE...WASAIDIZI WAKE WANATUMIA MUDA NA "MASOZI" NA WANA FAMILIA ZAO PIA VIPO VITENDEA KAZI HAVIKUSHUSHWA ZINGATIA. HATA HIVYO LABDA TUU TUNAWEZA KUSAHAU KUWA NA KILA MTENDA KAZI WA MADHABAHUNI ATAKULA MADHABAHUNI PAKE... HUYU BABA HII NDIYO MADHABAHU YAKE HIYO HATA HIVYO SIKUBALIANI KWAMBA KWA KIASI HICHI KIDOGO CHA FEDHA APATACHO NDIYO KWAMBA IWE NI MTU AUZAYE APATACHO BURE!!
JAMANI MBONA MAKASISI WENGI KATIKA NYUMBA ZA IBADA HUTOZA SADAKA/ZAKA NA MICHANGO MBALIMBALI NA MINGINE HUWA HATA NA "DEADLINE" NA UFUATILIJI MKUBWA SANA HUWA TUNAKUJA TUU NA KUTOA... AU WENGINE HUKO KWENU HAMTOIII? SIKU NYINGINE TUNAAMBIWA PANDA MBEGU KWA MUUJIZA WA OMBI HILI NA LILE NA TUNAAMINI WALA HATUNA SHIDA NA VITU VINATOKEA SOMETIMES!!
SIKU MOJA NILIANDIKA KUWA NAWAJUA WABONGO HATA HII MIA TANO WATAENDA KWA BABU NA KUTAKA KUBARGAIN BABU Ohh! MIE NINA MIA TATU TUU WAKATI KASHAPANDA GARI LA SH 170,000/= MPAKA SH 200,000/=

SWALA LA KUTAJA JINA LA YESU SINA UTHIBITISHO KAMA HATUMII JINA LA YESU KWENYE HUDUMA YAKE KAMA IMEKUWA NI KWAZO KWAMBA MTU AHITIMISHE KUWA NI 'roho' IDANGANYAYO.. KWANI KAMA UTAKUWA MSOMAJI WA MAANDIKO, nafikiri kutakuwa hakuna umakini kidogo hapo! gv a benefit of doubt!!
YESU MWENYEWE ALISEMA KUWA WATAKUJA "makristo" WENGI WAKIDANGANYA KWA JINA LAKE...SASA ANGEWEZA PIA KUSEMA HILI JINA LAKINI BADO AKAWA NI 'roho' IDANGANYAYO... HATA WEWE TU KWA KUTUMIA JINA LA YESU SI UTHIBITISHO KWA ULIMWENGU KUWA AT ONE POINT HUWEZI KUWA MDANGANYAJI...WOTE TUMEKOSA NA KUPUNGUKIWA NA UTUUFU WA MUNGU.. NAFAHAMU KUWA ANDIKO LINASEMA HAKUNA AWEZAYE KUSEMA KRISTO NI MWANA WA MUNGU ISIPOKUWA AMEWEZESHWA NA ROHO WA MUNGU... MAASKOFU WA ARUSHA NA MOSHI KKKT WALISHAFANYA UCHUNGUZI WA KINA KWANINI TUSIWAULIZE HAWA JUU YA DUKUDUKU ZETU?

LAANA ISIYO SABABU HAIMPATI MTU... PIA NASIKIA TUNAAMBIWA TUSILAANI SASA HAYA MAMBO YA KULAANIANA BADALA YA KUBARIKIANA YANATOKA WAPI?

NIAMINIVYO MIMI NI KWAMBA TULIVYOUMBWA MUNGU ALIRUHUSU KUJA NA KULA MICHE MITI NA MATUNDA YOTE YA KONDENI..IKIWA NA MAANA HIYO HUKO NDIYO KUNA VITU VYA AFYA ZETU NA KILA KITU SASA SI UNAJUA IPO MICHE MINGI SANA HATUIJUI SIUZE KUILA... HIVYO SI LAZIMA UKILA HIYO MICHE USEME JINA LA YESU... MAANA UNAWEZA KULISEMA HILO JINA ANY TIME LAKINI PIA HATUPASWI KULITAJA BURE... KILA MNYWAPO NA KULA NI KUSHUKURU TUU... NIMESIKIA WANAPOKUNYWA HIYO DAWA HUWA WANASALI SASA JEE NI HAPO HUWA HALITAJWI JINA LA YESU AU? NATAKA KUJUA KUWA AMESKIZISHWA AU NA YEYE ALIKWENDA HAKUSIKIA JINA LA YESU? AKAKWAZIKA!!

KUHUSU KUZIPIMA "roho" NAHITIMISHA HUYU BWANA Mchg wa Loliondo, KAMA HALIKANI JINA LA YESU KAMA ILIVYOSEMA... NA ANAENDELEA NA "THERAPY" YAKE KAMA KAWA NAMUONA TUU NI KAMA AKINA PAULO WALIVYOKUWA WANAWAAMBIA AKINA TIMO WANYWE ZABIBU KWA MATUMBO YAO AU YESU MWENYEWE ALIVYOPONYA KWA KUTUMIA VUMBI NA MATE, AU WALIOKUWA WANAKWENDA KUOGA KWENYE BIRIKA LA SOLOAM, AU KAMA NAAMANI ALIVYOAMBIWA AKANAWE KWENYE MAJI MAGADI AU NI CHUMVI VILE..any how what ever LAKINI IKUMBUKWE PIA KUWA WATU WANAWEZA
KUPONYWA KWA VITU VYA ASILI ALIVYOTUPA MUNGU NA NI KWA UWEZO WAKE TWAVIFANYA HIVI VYOTE... BINAFSI SIJAKUWA NA SHAKA SAANA ILA NAHITAJI SABABU ZA KUELEWEKA... MAANA HATA WEWE UKIPINGA TUU BILA UTHIBITISHO JE NA SISI TUKISEMA WEWE PIA NI "roho" IDANGANYAO HAPO INAKUWA AJE? TUTHIBITISHIE KWA NENO THABITI...
LABDA SWALI KWAMBA KWANINI NI YEYE MWENYEWE NDIYE ANAYETOA TIBA HIYO? JIBU= NDIYE ALIYEPAKWA MAFUTA,, UNAJUA WENGINE WAKIPEWA WATAKUWA KAMA YULE SAIMON MCHAWI ALIVYOTAKA KUTUMIA KIPAWA CHA ROHO KWA MATAKWA YAKE MWENYEWE NA CHA MOTO ALIKIONA ALIPOTAKA KUNUNUA ZILE NGUVU ZA ROHO Mtakata toka kwa KINA PETRO... KUMBUKA.

KAMA HUYU BWANA MCHG. WA LOLIONDO, HAYUPO KINYUME NASI BASI YUPO UPANDE WETU...AND VISE VERSA IT IS TRUE


TUTAZIPIMA KILA roho AIDHA ZINATOKA KIJIJINI, SHAMBANI, SHULENI, MAKAZINI, MIJINI na hata MADHABAHUNI!!! TUONE KAMA ZINATOKA KWA MUNGU.

BINAFSI NAAMINI KUWA HAKUNA JINA JINGINE LITUPASALO KUOKOLEWA KWALO ISIPOKUWA NI JINA LA YESU NA NINAAMINI HAUTUWEZI KUMWONA BABA ISIPOKUWA KWA NJIA AMBAYO NI HUYU YESU KRISTO WA NAZARETH AMBAYE KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU ALITUNGWA KWA MWANAMWALI MARIA "BIKIRA" NA KUZALIWA NA KUSULUBIWA AKAFA KWA MSALABA KUBEBA DHAMBI ZA ULIMWENGU... AKAWA MWOKOZI WETU... NA KWA KUMKIRI KWA KINYWA NA KUMWAMINI KWA KUWA MUNGU ALIMFUFUA KUTOKA KWA WAFU TUNAOKOKA... KWA HIYO NEEMA YAKE... NA PIA JINA HILO AMBALO KWALO TUNAWEKA MIKONO JUU YA WAGONJWA NA KUPATA AFYA NA WENYE PEPO NA KUFUNGULIWA... TUFUNGA NA KUFUNGUA VYA DUNIANI NA MBINGUNI KWA JINA HILO AMBALO HATA MILANGO YA KUZIMU INALIZIMIA KINOMANOMA...
KWA KUSEMA HAYA NATAKA NIKUTHIBITISHIE SINA SHIDA NA JINA...NIKUTOE WASIWASI TUU...
UKITAKA KUNISAIDIA NAPATIKANA Hapa hapaa
IM STAY TO BE CORRECTED...LET THE BALL ROLL ALL THE WAY FOR GOD'S GLORY...

Sunday, February 20, 2011

Kwa Ni Uinjilishaji wa Sasa Umekosa Dhamira Mathubuti?

ISAIAH 61:1-2
Daudi haikumsumbua kurudi porini baada ya kupakwa mafuta kuwa mfalme.
Je! ni kwanini?
Binafsi nafikiri daudi ilimlipasa aende kuonolewa ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kutumia kombeo, kumsifu Bwana kwa ustadi wote na kukamilishwa katika nguvu….
Apate:
1.Nidhamu,
2.Utii na
3.Dhamira ya Utumishi (Azma).
Kama Daudi Mfalme Angekuwa ni tunda ningesema alikuwa anavundikwa.
Nimeulizwa swali siku chache zilizopita na dada Faith Mmanywa Dk. kwamba ni kwanini nyakati hizi zetu hatuwashi moto wa INJILI kama wa akina
 
Alexander Dowie "Healing Apostle"
John G. Lake "A man of Healing"
Smith Wigglesworth "apostle of faith" & Kathryn Kuhlman "the woman who believed in miracles" Hawa wawili niliwasikia kwa mmoja kati ya ever best teacher back home. Bro.Mgisa Mtebe. Wewe kaka mgisa najua labda ungetamani unikataze lakini hutaweza kupingana na ukweli kwamba In God's order you are the best in area of teaching.
 
Wengine waliowasha moto huko nyuma ni akina
William Branham "Aman of Notable Signs and Wonders
William J Seymour "The catalyst of pentecost"
Charles F Perham "The father of Pentecost"
A.A. Allen "The miracle man"
Evan Robert "Welsh Revivalist"
 Wengine ni akina
John Wesley, Martin Luther,  Rev.Martin Luther King Jr, Billy Graham these gentlemen he's still operating till this dawn. he get older with ana amazing treasures.
Ebu jaribu hata kuwa-google tu hawa watu uone habari zao waweza kupata nini kiliwapeleka kwenye fanaka kubwa walizofikia. Nafikiri ukiangalia biograph zao ndiyo unaweza kuanzia...
Maana wote wameanza kwenye back ground tofauti wengine walitoka kwenye familia za kikristo wengine hata milango ya kanisa hawakuijua.. . Mfano mmoja mkali ni huyu jamaa anaitwa Asa Alonzo...huyu jamaa alikuwa anakwenda kulala "baby bottle of liquor" badala ya ile chupa ya maziwa yeye anapelekwa kulala na kilaji au supu ya mawe...kama ingekuwa ni kule mwanza ningesema ni tembo au ikong'o,,, na kule kiraracha ingekuwa ni ile mbeke kali "mbege" kama dada ni gongo kwa dengelua,, iringa ni ulanzi..... Huyu ni mmoja kati ya jamaa waliowasha moto mpaka mwaka 1970 alipotwaliwa kwenye maisha haya. Familia yake yaani Baba yake na mama yake walikuwa na liquor brew nyumbani.. ni kama pale kwenu iletwe kongagi company ikae sebuleni..ilikwa soo..
 
Hivyo yapo mambo mengi ya kujifunza ni kwanini we lag behind in perfomance.. ..
 
Je ni kukosa maono, maarifa,umakini" seriousness" au ujasiri?
 Wengine tunasema hatujaitiwa kufanya kazi ya muhubiri sasa ni ipi ile tuifanyayo.. . Hawa jamaa kule kale hawakuwa na via vingi vya utendeanji kazi kama sasa....wakina seymor walikuwa wanatumia meli kwenda maeneo kama south africa kuhubiri na  na garimoshi ndani ya uamerika na ilikuwa ni moto mkubwa kweli wa injili...australia na kwengineko.. ..
 
Ngoja niwe jugdmental kidogo.
I will speak to myself somtime so dont get uptight
Mini nafikiri huwa najiona kama bado muda kumbuka
"Procastination is stealing of time"
 
I can say i will do it tommorow remember
"Tomorrow had never come and it wont either"
 
Mara nyingine nasema kwamba bado sijapata hiki
Kumbuka "Usipokuwa mwanifu kwa kidogo ulichonacho iweje kwa mzinga"
Luka 19: 26 (Nawaambia kila aliye na kitu atapewa bali asiyenacho hata kile alichonacho ataporwa "atanyang'anywa" ) haya maneno aliyasema Mwana wa Mungu mwenyewe. Inagadhabisha kuona umepewa mbawa za kuruka kama mwewe halafu najifanya kobe kuingia majini..zitakatwa ehh!! halafu nikiwa kibubutu ndipo nitalijua jiji sawasawa mwanawane.
Zakayo hakufikiri mara mbili juu ya ufupi aliona resources kibao za kumwingiza Yesu sebuleni mwake na huyu jamaa alikuwa kama mgirigashi ya au mperizi yeyote yule kwa myaudi
 
Don't decieve your selves by situation that mingle around you, you will never get out of it if you wont do something over your mind.
 
You need to make a commitiment and be responsible for renewing of your mind
 
{I, anDy, i have to be renewed in my mind..that i can exel my spiritual gift that called by my name...In Jesus name.}
 
God deposited and invest a lot of potential in me, i have to get on fire..
I speak to my self in Jesus name.
 
The top priorities in my mind i bet are:
1. Discipline ...in the word of God
2. Obidience... in the word of God
3. Determination (Aspiration) ... in the word of God.
 
Hivi vitu vitatu hata katika maisha ya kawaida vyaweza kumfanya mtu akawa na mafanikio makubwa.... mimi huwa nawaangalia watu wa mlango wa pili yaani rafiki zangu au majirani amabo wamefanikiwa na kunizidi katika idara fulani fulani kimaisha nk naona ni hivi vitu wanakuwa wameng'ang'ana navyo. Hakuna hilahila au janja janja. Hila na janja janja has never live to last.
 

Discipline:
Katika Huduma, Shule, Kazini na katika Jamii discipline ni muhimu mno.
Nakumbuka hata shule ukiondoa nidhamu ya kusoma hakuna kufaulu iko wazi nasemea hii katika hali ya kawaida kabisa...
Kwa mfano: nakumbuka kuna nyakati nilikuwa shule nasoma kidizaini naona hapa nimeshaondoka kwenye nafasi ya kuanguka kwahiyo sikazi msuli kiivyo...matokeo yake unajikuta umekwenda lakini unapita na makarai.Cs'...kwi kwi kwi...Hi si nidhamu nzuri ya kusoma hata kidogo.....
We need excellence in the work of God." Wapo wanaosema Excellence is an attention to detail".... Hakuna kurara hakuna kurara.... Nidhamu ni ya msingi saana.
Sasa kama hakuna ufanisi katika kazi ya Mungu ni sawa na kuacha. Ila ukiwa na nidhamu utatamani kuwa fanisi.
Hili neno ndiyo lile lile aliloanza nalo Bwana yenu alipoanza huduma alianza Ku-Discipline watu kuwa Disciple-lize ahahaha sasa niseme aje Discipleshpling. Any way Kwenye Ministry ya TAFES wao ndio wanakaza kwenye misheni hii kubwa ya kutengeneza wanafunzi... .. Hili neno limetafsiriwa na wengi kwa namna nyingi na nyingi zina maana zinazolandana. ... kwa upande wangu Kudiscipline "Is to make people to be in a certain desired order of character that pertain persistence in constant manner as  followers and longing to learn right and share to others as well"  Ref anDysana
 
Obidience:
Hapa utakumbuka biblia inavyosema utii ni bora kuliko dhabihu au mafuta ya beberu.
Utii unafaa saana.. Wataalamu wanasema kuchelewa kutii ni sawa na kutotii!! mimi naikubali hii maana inafanana sawa kabisa na Dis-Obidience. ... Substute yake yaweza kuwa kiburi ambacho si majivuno. I have to be aware that if i'm lack in obdience i will miss-out my right portions.... So don't hang out from your staff...
Many define obidience very clear...Here im my view on a personal definition " It is self reliance of subjection that man has to a master or someone (like a friend or any person of highre degree) in responding  to an order at a right time in a right way no matter in what situations you're in, circumstances you're in or attitude that you posses at a moment, while you keep tha respect at high"
Ref. anDy saana
 
Kukurupuka hakuna faida, Walisubiri nguvu zikawajia  walivyochomoka huo moto uliowashwa haikuwa mchezo.... Nimesoma na hawa wazee akina Seymour walipokuwa wanaanza huduma zao huko Azusa CA kuna nyakati fire ziliikuja kwani watu walipiga simu Polisi kuwa kuna moto maana unaambiwa ile kama pentecost day ya kale ndivyo ilivyokuwa yaani ulikuwa unaonekana moto literal vichwani mwao.... si mchezo mwanangu baabaake mwenyewe. mtumishi wa bwana... Ujazo wake ni muhimu mno.
What happen ukikosa utii?
Unakosa Privilege... Kumbuka Ibrahim alivyoambiwa kumtoa mwanae isaka. Binafsi huwa namwangalia Ibrahimu kwenye Utii zaidi. Japo pia nakubali swala la msingi linalosemwa juu ya kuwa baba yetu wa Imani. Pasipo Utii hakuna utekelezaji wa Imani. Na Pasipo Imani huwezi kumpendeza Mungu. Kumbuka imani huja kwa kusikia na kusikia hukamilika kwa Utii. Mfano.Unaweza ukaitwa halafu matokeo yakawa tofauti:
1. Ukasikia,
2. Ukasikiliza,
3. Ukaitika,
Kusikia ni ile sauti (Empy Cymbal)
Kusikiliza ni kufuatilia maelezo (Listen)
Kuitika/ Kuitika Mwito hii siyo kusema naam au bee  (Responding to the order of the basic calling)
 
In a simple way Obidience it needs to have a positive interactions in conversartion btn master and servant
 
Let me describe one error that catch some of us:
Which is to explain our excusees in purpose of justify our disobidience!
Is very wrong and it can never be otherwise. wrongness needs changes to be right not maneuvering which lead to erroneous 
 
Iliwahi kumtokea Samuel alipokuwa anaitwa na Mungu.
Mwenye masikio na asikie
 
Determination:
Daniel, This is one of ICON i always admire his heart. dhamira/ kunuwia....kwake...very determinant person I had ever see
Daniel na akina Abednego walikuwa ni extremist to the opponent
Kwanza kabisa kunuia kuwa safi
 
 Mara nyingi hii hali watu huwa tunakuwa nayo tunapookoka kile kipindi cha awali usifanye mchezo.... Kama huu moto huufahamu muulize Peter Kitembe...One of My friend back in Dar...Yaani pale mbezi luis palivamiwa kwa hasira nakumbuka ile faragha ndogo ya pale mburahati ilikuwa hailewi somo... Nakumbuka akina Isaac Omary Wakati wako wachanga pamoja nami pia nilikuwa ni mchanga vilevile lakini kila mahala ulikuwa unajisikia kufanya kazi ya Bwana nakumbuka faragha ilikuwa mpaka inapeleka sadaka kule. Ilikuwa fire...
Biblia kwenye  Kitabu cha Mithali inasomeka hivi "nafsi yenye njaa huona hata kitu kichungu kuwa ni kitamu  bali nafsi iliyoshiba hukinai hata sega la asali"
Mimi nakwambia ukiwa na dhamira kuu ni kama aliyekuwa na njaa..... hata mtu aliyeokoka unafahamu kabisa kuwa kaokoka unaenda kumhakiki maana unafahamu kuwa Neno linasema si wote waniitao Bwana Bwana au aliyesimama na aangalie asije akaanguka. Huwezi kuridhika na kukaa kimya... Unajua saa ya wokovu si kesho ni sasa. (Bila kumwaga lulu kwenye nguruwe)
Hawa akina daniel hawakuogopa kifo kama akina Luther, Dowie huyu alikuwa ana Healing home yaani watu wanapona hakuna mfano lakini vitisho vya vifo vilivyolingana na wingi wa uponyaji wake ndiyo vilikuwa kichocheo kibubwa cha dhamira yake,, mwengine aliyeonyesha dhamira kubwa alikuwa  ni
Jack Coe..Private huyu alikuwa soo  walimuita "The man of reckless faith" mwaka 1956 huyu jamaa aliposikia kuwa Miami, Florida ndiyo sehemu ngumu saana kwa watimishi dhamira yake kuu akawa na shauku moja kubwa sana ya kwenda huko inadaiwa alipaata mafaniko makubwa saana katika uinjilishaji wake huko kuliko maeneo mengi aliyofanikiwa kwenda...Japo baadaye naye alitupwa jela huko florida... Kuna wanaodai kuwa alienda ili kujilinganisha na wengine kitu ambacho kinaweza kuwa na ukweli lakini Pia kuna Kitu cha kujifunza kuwa aggressive kwenye kazi ya kukomboa....
Kwenye waraka wa petro inasomeka hivi " Na wengine mtawaokoa kutoka katika moto"
Hapa ndipo lile neno la Bwana kwenye ufunuo juu ya Efeso linapopasa
Ufunuo 2:4 "Lakini nina neno juu yako kuwa umeuacha upendo wako wa Kwanza"
Upendo wa kwanza wenye dhamira njema...tukumbuke upendo wa kwanza. Upendo wa Kumpenda YESU wakati huo nakumbuka nina mistari minne nimeikariri najiona kama Morrice Cerullo...Yaani dhamira inakuwa driven na Imani kiasi kwamba huwezi kuamini hakuna atakayekataa kuokoka ukisham-tight na hiyo mistari... Kufunga na kuomba juu ya fulani siyo shida... Usifanye mchezo
 
How can you get into a fire with no a single burn?
Muulize Daniel? yeye aliingia...sasa leo tunaambiwa tuwaokoe wengine toka kwenye moto....
 
Hivi vitu vitatu vitakusaidia kuifahamu karama ya Mungu {Roho Mtakatifu} ndani yako na kuifanyia kazi maana ni ngumu kufanya kazi katika ofisi usiyo na taaluma nayo....kama sijaelewa hili ngoja nipitie wizara mbalimbali nikutane na waliongizwa wizara hizo kwa bahati mbaya ndiy nitajiju.... Maana kuna mawaziri wanalijiua jiji kweli..... huwa wanachekelea kwenye misharara tu hawapendi kama nini kuiona jumatatu inakuja... Hivyo kujua Karama yako si tu itakusaidia kufanya kazi basi itapunguza muda wako wa kubung'aa .. Kwani utaingia kwenye ofisi yako mara......
Nasikitika kujiona nachelewa kufanya kinachonihusu sijui wewe? Bla bla bla ..... zimenrudisha nyuma saana sizitaki tena.... Nilifikiri ni okey lakini siyo hata kidogo..... Itakuwaje sawa wakati nimepewa Roho na  tangazo la tumaini nami kama balozi niko kimya tuu.
Mhh no no no..
Many died and still we have some more who need a instantly rescue
Watu wanapotea si mchezo....Mungu atusaidie katika wakati mfinyu tulibaki nao uwe na maana kubwa. 
 
Harvest Time Walk Out... My Soul