Pageviews last month

Thursday, June 18, 2009

Harvest Time Walk Out... My Soul

ISAIAH 61:1-2
Daudi haikumsumbua kurudi porini baada ya kupakwa mafuta kuwa mfalme.
Je! ni kwanini?
Binafsi nafikiri daudi ilimlipasa aende kuonolewa ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kutumia kombeo, kumsifu Bwana kwa ustadi wote na kukamilishwa katika nguvu….
Apate:
1.Nidhamu,
2.Utii na
3.Dhamira ya Utumishi (Azma).
Kama Daudi Mfalme Angekuwa ni tunda ningesema alikuwa anavundikwa.
Nimeulizwa swali siku chache zilizopita na dada Faith Mmanywa Dk. kwamba ni kwanini nyakati hizi zetu hatuwashi moto wa INJILI kama wa akina

Alexander Dowie "Healing Apostle"
John G. Lake "A man of Healing"
Smith Wigglesworth "apostle of faith" & Kathryn Kuhlman "the woman who believed in miracles" Hawa wawili niliwasikia kwa mmoja kati ya ever best teacher back home. Bro.Mgisa Mtebe. Wewe kaka mgisa najua labda ungetamani unikataze lakini hutaweza kupingana na ukweli kwamba In God's order you are the best in area of teaching.

Wengine waliowasha moto huko nyuma ni akina
William Branham "Aman of Notable Signs and Wonders
William J Seymour "The catalyst of pentecost"
Charles F Perham "The father of Pentecost"
A.A. Allen "The miracle man"
Evan Robert "Welsh Revivalist"
Wengine ni akina
John Wesley, Martin Luther, Rev.Martin Luther King Jr, Billy Graham this gentleman he's still operating till this dawn. he get older with ana amazing treasures.
Ebu jaribu hata kuwa-google tu hawa watu uone habari zao waweza kupata nini kiliwapeleka kwenye fanaka kubwa walizofikia. Nafikiri ukiangalia biograph zao ndiyo unaweza kuanzia...
Maana wote wameanza kwenye back ground tofauti wengine walitoka kwenye familia za kikristo wengine hata milango ya kanisa hawakuijua.. . Mfano mmoja mkali ni huyu jamaa anaitwa Asa Alonzo...huyu jamaa alikuwa anakwenda kulala "baby bottle of liquor" badala ya ile chupa ya maziwa yeye anapelekwa kulala na kilaji au supu ya mawe...kama ingekuwa ni kule mwanza ningesema ni tembo au ikong'o,,, na kule kiraracha ingekuwa ni ile mbeke kali "mbege" kama dada ni gongo kwa dengelua,, iringa ni ulanzi..... Huyu ni mmoja kati ya jamaa waliowasha moto mpaka mwaka 1970 alipotwaliwa kwenye maisha haya. Familia yake yaani Baba yake na mama yake walikuwa na liquor brew nyumbani.. ni kama pale kwenu iletwe kongagi company ikae sebuleni..ilikwa soo..

Hivyo yapo mambo mengi ya kujifunza ni kwanini we lag behind in perfomance.. ..

Je ni kukosa maono, maarifa,umakini" seriousness" au ujasiri?
Wengine tunasema hatujaitiwa kufanya kazi ya muhubiri sasa ni ipi ile tuifanyayo.. . Hawa jamaa kule kale hawakuwa na via vingi vya utendeanji kazi kama sasa....wakina seymor walikuwa wanatumia meli kwenda maeneo kama south africa kuhubiri na na garimoshi ndani ya uamerika na ilikuwa ni moto mkubwa kweli wa injili...australia na kwengineko.. ..

Ngoja niwe jugdmental kidogo.
I will speak to myself somtime so dont get uptight
Mini nafikiri huwa najiona kama bado muda kumbuka
"Procastination is stealing of time"

I can say i will do it tommorow remember
"Tomorrow had never come and it wont either"

Mara nyingine nasema kwamba bado sijapata hiki
Kumbuka "Usipokuwa mwanifu kwa kidogo ulichonacho iweje kwa mzinga"
Luka 19: 26 (Nawaambia kila aliye na kitu atapewa bali asiyenacho hata kile alichonacho ataporwa "atanyang'anywa" ) haya maneno aliyasema Mwana wa Mungu mwenyewe. Inagadhabisha kuona umepewa mbawa za kuruka kama mwewe halafu najifanya kobe kuingia majini..zitakatwa ehh!! halafu nikiwa kibubutu ndipo nitalijua jiji sawasawa mwanawane.
Zakayo hakufikiri mara mbili juu ya ufupi aliona resources kibao za kumwingiza Yesu sebuleni mwake na huyu jamaa alikuwa kama mgirigashi ya au mperizi yeyote yule kwa myaudi

Don't decieve your selves by situation that mingle around you, you will never get out of it if you wont do something over your mind.

You need to make a commitiment and be responsible for renewing of your mind

{I, anDy, i have to be renewed in my mind..that i can exel my spirtual gift that called by my name...In Jesus name.}

God deposited and invest a lot of pontentila in me, i have to get on fire..
I speak to my self in Jesus name.

The top priorities in my mind i bet are:
1. Discipline ...in the word of God
2. Obidience... in the word of God
3. Determination (Aspiration) ... in the word of God.


Hivi vitu vitatu hata katika maisha ya kawaida vyaweza kumfanya mtu akawa na mafanikio makubwa.... mimi huwa nawaangalia watu wa mlango wa pili yaani rafiki zangu au majirani ambao wamefanikiwa na kunizidi katika idara fulani fulani kimaisha nk naona ni hivi vitu wanakuwa wameng'ang'ana navyo. Hakuna hilahila au janja janja. Hila na janja janja can never live to last.

Discipline:
Katika Huduma, Shule, Kazini na katika Jamii discipline ni muhimu mno.
Nakumbuka hata shule ukiondoa nidhamu ya kusoma hakuna kufaulu iko wazi nasemea hii katika hali ya kawaida kabisa...
Kwa mfano: nakumbuka kuna nyakati nilikuwa shule nasoma kidizaini naona hapa nimeshaondoka kwenye nafasi ya kuanguka kwahiyo sikazi msuli kiivyo...matokeo yake unajikuta umekwenda lakini unapita na makarai.Cs' ...kwi kwi kwi...Hi si nidhamu nzuri ya kusoma hata kidogo.....
We need excellence in the work of God." Wapo wanaosema Excellence is an attention to detail".... Hakuna kurara hakuna kurara.... Nidhamu ni ya msingi saana.
Sasa kama hakuna ufanisi katika kazi ya Mungu ni sawa na kuacha. Ila ukiwa na nidhamu utatamani kuwa fanisi.
Hili neno ndiyo lile lile aliloanza nalo Bwana yenu alipoanza huduma alianza Ku-Discipline watu kuwa Disciple-lize ahahaha sasa niseme aje Discipleshpling. Any way Kwenye Ministry ya TAFES wao ndio wanakaza kwenye misheni hii kubwa ya kutengeneza wanafunzi... .. Hili neno limetafsiriwa na wengi kwa namna nyingi na nyingi zina maana zinazolandana. ... kwa upande wangu Kudiscipline "Is to make people to be in a certain desired order of character that pertain persistence in constant manner as followers and longing to learn right and share to others as well" Ref anDysana

Obidience:
Hapa utakumbuka biblia inavyosema utii ni bora kuliko dhabihu au mafuta ya beberu.
Utii unafaa saana.. Wataalamu wanasema kuchelewa kutii ni sawa na kutotii!! mimi naikubali hii maana inafanana sawa kabisa na Dis-Obidience. ... Substute yake yaweza kuwa kiburi ambacho si majivuno. I have to be aware that if i'm lack in obdience i will miss-out my right portions.... So don't hang out from your staff...
Many define obidience very clear...Here im my view on a personal definition " It is self reliance of subjection that man has to a master or someone (like a friend or any person of highre degree) in responding to an order at a right time in a right way no matter in what situations you're in, circumstances you're in or attitude that you posses at a moment, while you keep tha respect at high"
Ref. anDy saana

Kukurupuka hakuna faida, Walisubiri nguvu zikawajia walivyochomoka huo moto uliowashwa haikuwa mchezo.... Nimesoma na hawa wazee akina Seymour walipokuwa wanaanza huduma zao huko Azusa CA kuna nyakati fire ziliikuja kwani watu walipiga simu Polisi kuwa kuna moto maana unaambiwa ile kama pentecost day ya kale ndivyo ilivyokuwa yaani ulikuwa unaonekana moto literal vichwani mwao.... si mchezo mwanangu baabaake mwenyewe. mtumishi wa bwana... Ujazo wake ni muhimu mno.
What happen ukikosa utii?
Unakosa Privilege... Kumbuka Ibrahim alivyoambiwa kumtoa mwanae isaka. Binafsi huwa namwangalia Ibrahimu kwenye Utii zaidi. Japo pia nakubali swala la msingi linalosemwa juu ya kuwa baba yetu wa Imani. Pasipo Utii hakuna utekelezaji wa Imani. Na Pasipo Imani huwezi kumpendeza Mungu. Kumbuka imani huja kwa kusikia na kusikia hukamilika kwa Utii. Mfano.Unaweza ukaitwa halafu matokeo yakawa tofauti:
1. Ukasikia,
2. Ukasikiliza,
3. Ukaitika,

Kusikia ni ile sauti (Empy Cymbal)
Kusikiliza ni kufuatilia maelezo (Listen)
Kuitika/ Kuitika Mwito hii siyo kusema naam au bee (Responding to the order of the basic calling)

In a simple way Obidience it needs to have a positive interactions in conversartion btn master and servant

Let me describe one error that catch some of us:
Which is to explain our excusees in purpose of justify our disobidience!
Is very wrong and it can never be otherwise. wrongness needs changes to be right not maneuvering which lead to erroneous

Iliwahi kumtokea Samuel alipokuwa anaitwa na Mungu.
Mwenye masikio na asikie

Determination:
Daniel, This is one of ICON i alwasy admire his heart. dhamira/ kunuwia....
Daniel na akina Abednego walikuwa ni extremst to the opponent
Kwanza kabisa kunuia kuwa safi

Mara nyingi hii hali watu huwa tunakuwa nayo tunapookoka kile kipindi cha awali usifanye mchezo.... Kama huu moto huufahamu muulize Peter Kitembe...One of My friend back in Dar...Yaani pale mbezi luis palivamiwa kwa hasira nakumbuka ile faragha ndogo ya pale mburahati ilikuwa hailewi somo... Nakumbuka akina Isaac Omary Wakati wako wachanga pamoja nami pia nilikuwa ni mchanga vilevile lakini kila mahala ulikuwa unajisikia kufanya kazi ya Bwana nakumbuka faragha ilikuwa mpaka inapeleka sadaka kule. Ilikuwa fire...
Biblia kwenye Kitabu cha Mithali inasomeka hivi "nafsi yenye njaa huona hata kitu kichungu kuwa ni kitamu bali nafsi iliyoshiba hukinai hta sega la asali"
Mimi nakwambia ukiwa na dhamira kuu ni kama aliyekuwa na njaa..... hata mtu aliyeokoka unafahamu kabisa kuwa kaokoka unaenda kumhakiki maana unafahamu kuwa Neno linasema si wote waniitao Bwana Bwana au aliyesimama na aangalie asije akaanguka. Huwezi kuridhika na kukaa kimya... Unajua saa ya wokovu si kesho ni sasa. (Bila kumwaga lulu kwenye nguruwe)
Hawa akina daniel hawakuogopa kifo kama akina Luther, Dowie huyu alikuwa ana Healing home yaani watu wanapona hakuna mfano lakini vitisho vya vifo vilivyolingana na wingi wa uponyaji wake ndiyo vilikuwa kichocheo kibubwa cha dhamira yake,, mwengine aliyeonyesha dhamira kubwa alikuwa ni
Jack Coe..Private huyu alikuwa soo walimuita "The man of reckless faith" mwaka 1956 huyu jamaa aliposikia kuwa Miami, Florida ndiyo sehemu ngumu saana kwa watimishi dhamira yake kuu akawa na shauku moja kubwa sana ya kwenda huko inadaiwa alipaata mafaniko makubwa saana katika uinjilishaji wake huko kuliko maeneo mengi aliyofanikiwa kwenda...Japo baadaye naye alitupwa jela huko florida... Kuna wanaodai kuwa alienda ili kujilinganisha na wengine kitu ambacho kinaweza kuwa na ukweli lakini Pia kuna Kitu cha kujifunza kuwa aggressive kwenye kazi ya kukomboa....
Kwenye waraka wa petro inasomeka hivi " Na wengine mtawaokoa kutoka katika moto"
Hapa ndipo lile neno la Bwana kwenye ufunuo juu ya Efeso linapopasa
Ufunuo 2:4 "Lakini nina neno juu yako kuwa umeuacha upendo wako wa Kwanza"
Upendo wa kwanza wenye dhamira njema...tukumbuke upendo wa kwanza. Upendo wa Kumpenda YESU wakati huo nakumbuka nina mistari minne nimeikariri najiona kama Morrice Cerullo...Yaani dhamira inakuwa driven na Imani kiasi kwamba huwezi kuamini hakuna atakayekataa kuokoka ukisham-tight na hiyo mistari... Kufunga na kuomba juu ya fulani siyo shida... Usifanye mchezo

How can you get into a fire with no a single burn?
Muulize Daniel? yeye aliingia...sasa leo tunaambiwa tuwaokoe wengine toka kwenye moto....

Hivi vitu vitatu vitakusaidia kuifahamu karama ya Mungu {Roho Mtakatifu} ndani yako na kuifanyia kazi maana ni ngumu kufanya kazi katika ofisi usiyo na taaluma nayo....kama sijaelewa hili ngoja nipitie wizara mbalimbali nikutane na waliongizwa wizara hizo kwa bahati mbaya ndiy nitajiju.... Maana kuna mawaziri wanalijiua jiji kweli..... huwa wanachekelea kwenye misharara tu hawapendi kama nini kuiona jumatatu inakuja... Hivyo kujua Karama yako si tu itakusaidia kufanya kazi basi itapunguza muda wako wa kubung'aa .. Kwani utaingia kwenye ofisi yako mara......
Nasikitika kujiona nachelewa kufanya kinachonihusu sijui wewe? Bla bla bla ..... zimenrudisha nyuma saana sizitaki tena.... Nilifikiri ni okey lakini siyo hata kidogo..... Itakuwaje sawa wakati nimepewa Roho na tangazo la tumaini nami kama balozi niko kimya tuu.
Mhh no no no..
Many died and still we have some more who need a instantly rescue
Watu wanapotea si mchezo....Mungu atusaidie katika wakati mfinyu tulibaki nao uwe na maana kubwa.